Ijumaa, 6 Januari 2017

POSTED 9 HOURS AGO DESKTOP VIEW BACK TO TOP SOKA Mfaransa Yanga SC awachomoka Simba Jerome Dofourg By GIFT MACHA, UNGUJA IN SUMMARY ‘‘Tangu nije, nimetengwa katika maamuzi na harakati za klabu, sijakuwa na mazingira mazuri ya kufanya kazi kabla ya uamuzi huo. Nawatakia kila la heri Yanga nikisaka riziki kwingine.’’ ADVERTISEMENT ADVERTISEMENT YANGA imeamua kusitisha rasmi cheo cha Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa klabu. Tafsiri rahisi ni kwamba Mfaransa, Jerome Dofourg hana chake na hata Simba na Yanga zikikutana wikiendi ijayo kwenye Kombe la Mapinduzi huenda asiwepo kabisa kama Yusuf Manji akisaini cheki yake ya malipo mapema. “Nimeambiwa nisepe zangu kwa kuwa Yanga Yetu haipo tena kwani serikali imesimamisha mradi huo. Natarajia kumalizana na mabosi wangu kabla ya kurejea nyumbani Ufaransa wiki ijayo, alisema Dufourg katika mahojiano ya kipekee na Mwanaspoti. ‘‘Tangu nije, nimetengwa katika maamuzi na harakati za klabu, sijakuwa na mazingira mazuri ya kufanya kazi kabla ya uamuzi huo. Nawatakia kila la heri Yanga nikisaka riziki kwingine.’’ Jerome aliletwa nchini na Kampuni ya Yanga Yetu Limited ambayo ilikuwa imeidhinishwa na bodi ya wadhamini ya Yanga na wanachama kuikodi klabu hiyo kwa miaka 10 mfululizo kuanzia Septemba mwaka jana. Lakini baadaye Serikali kupitia Baraza la Michezo ilisitisha ukodishwaji wa Yanga kwa maelezo kwamba mchakato huo ni mrefu na unahitaji kufuata taratibu na si kukurupuka. Hatua hiyo ilisababisha kusitishwa kwa shughuli zote za Yanga Yetu Limited iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imejiridhisha nazo ni kwamba hata Jerome ameambiwa hana chake kwavile mchakato umeshindikana. Ingawa bado inafanywa siri, lakini habari za ndani ambazo Mwanaspoti inazo ni kwamba Jerome ameambiwa kwamba ajira yake haitakuwepo kwavile mchakato umesitishwa na ngazi za juu. “Kwa sasa anasubiri tu malipo yake ya kusitisha mkataba pamoja na tiketi arudi kwao, kwavile Yanga Yetu ambayo yeye ndiye alipaswa kuiendesha imekataliwa kuikodisha Yanga,” kilisema chanzo chetu. Habari zinasema kwamba Jerome ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja tangu Oktoba, amekuwa akiwalalamikia viongozi kutokana na kutohusishwa kwenye maamuzi ya kila siku ya utendaji wa klabu kinyume na mkataba wake. Jambo ambalo liliwalazimu wasaidizi wa Manji kumwambia wazi kwamba ajira yake imesitishwa kwavile Yanga Yetu haipo na habari zinadai kwamba amekubaliana na hali halisi na sasa amepumzika kwenye hoteli moja ya ufukweni Dar es Salaam akingoja chake ili asepe wikiendi ijayo. SIKIA HII Ingekuwa kwenye familia, Jerome angelazimika kuwasalimia wachezaji wote wakubwa wa Yanga akiwemo Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Justine Zulu, Thabani Kamusoko kwavile wamemzidi umri kwani ana miaka 29 tu. Mtaalamu huyo kama angedumu Yanga kazi yake ilikuwa kusimamia mradi wa Yanga Yetu na kuigeuza klabu hiyo iwe ya kibiashara zaidi. Kwa mujibu wa mkataba wa kukodishwa kwa Yanga, Manji angepewa timu ya soka na nembo ya klabu. Mzungu huyo ana vyeti vya usimamizi wa biashara na utawala, fedha, mahusiano ya kitaifa na mikakati ya biashara. Amefanya kazi Kenya, Rwanda, Dubai na Umoja wa Falme za Kiarabu. WALETE SIMBA Wakati Mfaransa akiondoka, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi ametamka mjini Unguja kwamba hawana wasiwasi wa kukutana na watani zao Simba katika hatua ya nusu fainali kwani awamu hii wamejipanga na wanazipa heshima sawa timu zote. “Huwezi kuja katika mashindano halafu useme kwamba hujajiandaa kucheza na timu fulani, hapana. Tunazipa uzito timu zote hapa na haijalishi tutakutana na timu gani katika nusu fainali. “Hata kama tutakutana na Simba si mbaya, ni jambo la kawaida kwetu, tunajipanga kwaajili ya kufanya vizuri katika

Show love

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni